Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa zoezi la usajili wa kadi za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.

Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa zoezi la usajili wa kadi za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole Mei mosi mwaka huu, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wameonyesha wasiwasi kuwa huenda watashindwa kupata huduma hiyo kutokana na kutokuwa na vitambulisho vya Taifa ambavyo vitatumika katika usajili huo.

Wakizungumza na Channel Ten wamesema zoezi hilo ni zuri na huenda likawa ndio mwarobaini wa uhalifu mitandaoni lakini wapo baadhi ya wannachi ambao bado hawana vitambulisho ya taifa, hivyo wameiomba mamlaka husika kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.

Aidha wamezungumzia changamoto ya gharama za matumizi ya simu kwa madai kuwa ndizo zimekuwa zikiwalazimu kumiliki kadi zaidi ya moja. Usajili huu mpya unahitaji mteja kuwa na kadi moja pekee kwa kila mtandao.

John Dafa ni Mkurugenzi wa usajili na ufuatiliaji Mamlaka ya mawasiliano Tanzania – TCRA anaeleza namna ambavyo usajili utafanyika akisisitiza kuwa usajili hautakuwa wa mashaka na tayari wamewasiliana na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA kwamba itatoa namba kwa wale ambao tayari wamejiandikisha lakini bado hawajapa vitambulisho hivyo.

Comments

comments