Waziri Prof. Joyce Ndalichako azindua Chuo cha VETA Urambo.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetenga kiasi cha sh. Billion arobaini kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi VETA, hatua ambayo itawasaidia vijana wengi kupata ujuzi na stadi katika fani mbalimbali ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano iliyojikita katika maendeleo yanayotokana na uchumi wa Viwanda.

Akizindua chuo cha mafunzo ya ufundi stadi VETA wilayani Urambo waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema chuo hiki ni fursa kwa vijana katika kupata ujuzi huku akisisitiza kutunza miundo mbinu hii ambayo imegharimu pesa nyingi.

Miongoni mwa malengo ya VETA ni kuendelea kufanya ubunifu utakaosaidia katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo.

Comments

comments