Waziri mkuu Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya uchunguzi wa mionzi yenye viwango vya kimataifa.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa serikali wa kujenga maabara ya kisasa ya uchunguzi wa mionzi yenye viwango vya kimataifa ni kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama wa nchi na mipaka yake yote dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa hapa nchini kupitia mionzi.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi ya maabara hiyo katika makao makuu ya tume ya mionzi jijini Arusha iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zilizotolewa na serikali ya Tanzania,ambayo imesheheni vifaa vya kisasa vyenye thamani ya shilingi bilioni 7.5 zilizotolewa na Jumuiya ya Ulaya.

Amesema hatua hiyo ni mwanzo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya kuimarisha usalama katika matumizi ya teknolojia za kisasa zinazoweza kuingizwa hapa nchini na kuleta madhara kwa wananchi na mazingira.

Mwenyeki wa bodi ya tume ya mionzi Dkt. Najat Mohamed amemweleza waziri mkuu kuwa licha ya watendaji wa taasisi hiyo kukabiliwa na vishawishi vya rushwa kutoka kwa watendaji wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakifanyakazi kwa weledi ili kunusuru maisha ya watanzania na chi kwa ujumla.

Mapema leo asubuhi kabla ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa kuzindua maabara hiyo alifungua mkutano wa wataalam wa nyuklia kutoka nchi 20 za SADC unaojadili namna ya kuimarisha usalama katika matumizi ya technolojia hiyo.

Comments

comments