Wazalishaji Mifuko mbadala watakiwa kuomba Leseni.

Shirika la Viwango Tanzania TBS limewataka wazalishaji wote wa mifuko mbadala pamoja na waagizaji wa mifuko hiyo kutoka nje kuwasilisha upya maombi ya kupatiwa leseni, baada ya shirika hilo kusitisha uhuishaji wa leseni za awali zilizoruhusu uzalishaji wa mifuko ya plastiki.

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika hilo Bw. Lazaro Msalalaga amesema hatua hiyo pia iambatane na kuthibitisha ubora wa mifuko mbadala inayozalishwa kwa sasa na ambayo ipo sokoni kwa matumizi, ili kuhakikisha kuwa inakidhi matakwa ya kumlinda mtumiaji.

Amesema kulingana na agizo la serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, TBS imeandaa viwango vipya viwili kwa ajili ya uzalishaji wa mifuko mbadala ikiwemo ya karatasi, nguo, gunia na vikapu, ambavyo malighafi yake haina chembe chembe za plastiki. Viwango hivyo ni TZS 2292 na TZS 2130 vya mwaka 2018.

Comments

comments