Watu watatu wanaswa na Meno ya Tembo Songwe.

Watu watatu, wawili wakiwa raia wa nchi jirani ya Malawi ,wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na vipande 17 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogram 33 pamoja na kuwakamata watu wanne wakituhumiwa kwa mauaji ya watu wawili waliowaua na kuwacharanga na mapanga.

Akizungumza na Channel Ten ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani,Songwe, George Kyando amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika kijiji cha Lungwe B wilaya ya ileje mpakani na nchi jirani ya Malawi ikidaiwa kuwa meno hayo yametolewa nchini Malawi.

Aidha kamanda Kyando amesema kuwa watuhumiwa wawili ni raia wa Tanzania na mmoja ni raia wa Malawi na mzigo huo ulikutwa kwenye nyumba ya mtanzania chumbani kwake.

Hata hivyo kamanda Kyando amesema jeshi lake pia limewakamata watu wanne wakituhumiwa kwa mauaji ya watu wawili wilayani Momba na Mbozi ambao walikuwa wamekatwa kichwa ,mikono na tumbo.

Kamanda Kyando ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Songwe kutoa taarifa ya bishara hizo haramu pamoja na matukio Mbalimbali ya kihalifu akisema jeshi la polisi litendelea kupambana kuhakikisha mkoa unakuwa salama.

Comments

comments