Watu watatu raia wa kigeni wamepandishwa kizimbani Mbeya.

Watu watatu raia wa kigeni kutoka nchi za Ireland na Uingereza wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na madini aina ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 98 kinyume na sheria na taratibu za nchi.

Akisoma Shitaka Mwendesha Mashitaka wakili Msomi wa Serikali Mwandamizi Jacqueline Nyantori, anasema washitakiwa hao kwa pamoja wametenda kosa hilo la uhujumu uchumi Julai tatu mwaka huu na kukamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe uliopo Mkoani Mbeya ambapo walikutwa na madini aina ya yenye uzito wa gram 1043.33 yenye thamani ya shilingi milioni 98.5 .

Wakili huyo amewataja washitakiwa hao kuwa ni Clive Rooney (62) raia wa nchi ya Irish ambaye ni Meneja wa fedha, Ross Harris (34) na Robert Wheedon (59)ambao ni raia wa nchini uingereza ambapo wamekamatwa na madini hayo wakiyasafirisha kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Mwendesha mashitaka wa serikali nasema washitakiwa hao wamekamatwa na Madini kinyume cha Sheria ya Uhujumu uchumi namba 18 (1) na 4 kifungu cha (1a) na kifungu cha sheria ya madini namba 14 cha mwaka 2010, ikiwa ni pamoja na aya ya 27 ya jedwali la kwanza na kifungu namba 57 kifungu kidogo.

Aidha Kaimu Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya Venance Mulingi amesema Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shitaka hili ambapo washitakiwa wamerudishwa wamerudishwe rumande hadi Julai 22 mwaka huu.

Comments

comments