Watanzania wamekumbushwa kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Taifa.

Wakati Tanzania ikiendelea kutekeleza sera ya viwanda inayolenga kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, watanzania wamekumbushwa kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Taifa, ili kuliwezesha Taifa kunufaika kiuchumi na rasilimali hizo.

Ushauri huo umetolewa na jopo la wahariri wa vyombo mbalimbali habari nchini, baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Saanane Jijini Mwanza, ambacho kinamilikiwa na hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA).

Unapohitaji kutembelea hifadhi ya kisiwa hicho, unalazimika kupanda boti ya mwendo kasi, itakayokuwezesha kushuhudia vivutio mbalimbali vilivyopo katika kisiwa hicho, lakini pia mandhari nzuuri ya Jiji la Mwanza.

Hamisi Salum ni mwongoza watalii katika hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.

Jopo la wahariri na waandishi wa habari waandamizi, limetembelea hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, baada ya kukamilisha mkutano uliolikutanisha jopo hilo na uongozi wa wa (TANAPA), kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha sekta ya utalii nchini.

Comments

comments