Wananchi watakiwa kulinda Maliasili.

Katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira unayoyakabili baadhi ya maeneo ya hifadhi za Taifa, Wizara ya maliasili na utalii imewataka wananchi kulinda maliasili na hifadhi zinazowazunguka, ili kuviwezesha vizazi vya sasa na vijavyo kunufaika na rasilimali hiyo.

Wizara hiyo imetoa agizo hilo leo Jijini Mwanza, kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya wizara Dkt. Hamis Kigwangala.

Sekta ya utalii na uhifadhi ni nguzo mhimu ya maendeleo ya Taifa, kwa kuwa inachangia kuinua uchumi wa Taifa kupitia fedha za kigeni, kutokana na rasilimali za wanyamapori na mazingira zinazopatikana ndani ya hifadhi hizo.

Akifungua mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa na wahariri pamoja na waandishi wa habari waanamizi, Waziri wa maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangala, amewashauri waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuielimisha jamii lakini pia kutangaza vivutio vya Taifa.

Kutokana na umuhimu wa sekta ya uhifadhi na utalii, Kamishna wa shirika la hifadhi Tanzania (TANAPA) Dkt. Alan Kijazi, amesema wamekuwa wakitambua michango inayotolewa na vyombo vya habari katika kuhamasisha utalii wa ndani.

Comments

comments