Wananchi wametakiwa kutumia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa.

Wananchi wametakiwa kutumia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kama fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vya kuzalisha mifuko mbadala hatua ambayo itasaidia kuwapatia kipato na hatimaye kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya mifukpo hiyo.

Kutokana na madhara kadha wa kadha yanayotokana na matuimizi ya mifuko ya plastic ikiwa ni pamoja na kusababisha uharibifu wa mazingira pamoja na uchafuzi wa mazingira hali iliyosababisha katazo dhidi ya matumizi ya mifuko hiyo mara tu ifikapo tarehe moja mwezi june, wananchi wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia fursa hii itakayowasaidia kujiopatia kipato.

Licha ya uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya mifuko ya plastiki mifuko hii pia imekuwa ikisababisha vifo vya mifugo kama wanavyobainisha baadhi ya Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga.

Hata hivyo jitihada hizi zimeonesha kuungwa mkono na wafanya biashata wilayani igunga kwa kuzalisha vifungashio.

Comments

comments