Wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Uhuru Media Group wametembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Chama Cha Mapinduzi – CCM.

Wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Uhuru Media Group wakiongozwa na mwenyekiti wa bodi hiyo Rodrick Mpogolo wametembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Chama Cha Mapinduzi – CCM ikiwemo Gazeti la Uhuru, Radio Uhuru, Channel Ten na Radio Magic, jijini Dar es Salaam jana.

Bodi hiyo ambayo imeteuliwa hivi karibuni imefanya ziara hiyo kwa lengo la kuangalia namna ambavyo vyombo hivyo vinatekeleza majukumu yake pamoja na kufahamu changamoto zinazowakabili ili kujipanga namna ya kukabiliana nazo.

Akizungumza akiwa katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Rodrick Mpogolo amesema vyombo vya habari vya chama cha Mapinduzi vina jukumu la kurithisha mazuri yaliyofanywa na viongozi waliopita katika awamu zote lakini pia kuwakumbusha vijana historia ya Taifa hili kwani vijana wa sasa hawafahamu nchi ilikotoka.

Rodrick Mpogolo – Mwenyekiti wa Bodi UMGL

Wakiwa katika ofisi za gazeti la uhuru walipata fursa ya kujionea gazeti la mwaka 1961 jambo ambalo amesema linadhihirisha ukongwe wa chombo hicho hivyo kazi kubwa ya bodi hiyo ni kuelekeza nguvu katika kuviwezesha vyombo vya chama kufanya kazi kuisaidia serikali kufikisha taarifa ya kazi nzuri inayofanywa na serikali kwa watanzania.

Wakiwa katika studio za Radio Magic wajionea jinsi wafanyakazi walivyo na ari ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo utoaji wa Burudani.

Comments

comments