Utoaji wa Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Serikali imeombwa kuongeza kasi ya utoaji chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo limeonekana kuwa tishio kwa wanawake hapa nchini.

Ombil hilo limetolewa na wanawake wa Manispaa ya Singida katika uzinduzi wa zoezi la uchunguzi wa saratani ya awali ya matiti,shingo ya kizazi pamoja tezi dume uliofanyika mjini Singida ambapo wanawake wa Manispaa ya Singida wakahimiza kuhusu utoaji wa chanjo hiyo.

Awali,akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la uchunguzi wa saratani ya awali ya matiti,shingo ya kizazi pamoja na tezi dume mjini Singida,Meneja wa Kitemgo cha Saratani kutoka Taasisi ya Ocean Road ya jijini Dar-es-Salaam.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt Anjelina Lutambi akahimiza juu ya wananchi wa Mkoa wa Singida kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kujua iwapo wapo salama au wameshapata saratani ili waweze kupata tiba mapema kabla ya kupata athari kubwa zaidi.

Comments

comments