Upanuzi wa gati namba moja la kupokelea meli katika bandari ya Dar es Salaam lenye uwezo wa kupokea meli mbili kwa wakati mmoja umekamilika kwa asilimia mia moja huku meli zikitarajia kuanza kutia nanga

Upanuzi wa gati namba moja la kupokelea meli katika bandari ya Dar es Salaam lenye uwezo wa kupokea meli mbili kwa wakati mmoja umekamilika kwa asilimia mia moja huku meli zikitarajia kuanza kutia nanga katika gati hilo baada ya wiki moja kuanzia sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ya Dar es Salaam mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini Mhandisi Deusdediti Kakoko amesema kuwa upanuzi wa gati namba moja umekamilika kwa asilimia mia moja na kwamba meli zitaanza kutia nanga baada ya wiki moja huku uwezo wake ukiwa ni kupokea meli kubwa mbili kwa wakati mmoja zenye uwezo wa kubeba tani elfu arobaini na tano hadi elfu sitini.

Aidha mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Fred Liundi amesema kuwa serikali iliamua kutumia zaidi ya shilingi 336.7 ili kuipa uwezo bandari hiyo kuhudumia shehena kubwa za mizigo.

Tazama Video hapa Chini;

Comments

comments