Ujenzi wa Ofisi za Walimu DSM, CRDB yakabidhi hundi ya Shs Milioni 100 kwa kamati

MAKONDA CRDB

Katika kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na kamati ya Ujenzi wa ofisi 402 za walimu na Vyoo Benki ya CRDB leo imekabidhi hundi ya shilingi Millioni mia moja kwa ajili ya Kuunga mkono ujenzi ofisi za walimu katika Mkoa wa Dsm.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt.Charles Kimei akizungumza kabla ya kukabidhi hundi amesema ameguswa na Kampeni hiyo ya ujenzi wa ofisi za walimu pamoja na ubunifu wenye tija unaofanywa na Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Paul Makonda katika kushughulikia kero mbali mbali za wananchi na watumishi wa umma wakiwemo walimu mkoani Dar es Salaam.

Amesema kwa kuanzia wanakabidhi shilingi millioni mia moja, lakini ameaahidi kutoa kiasi cha shilingi millioni mia moja nyingine mwezi Januari mwakani huku akihamasisha wananchi wanaotumia benki hiyo kujitokeza na kujitolea kuchangia ujenzi huo.

Katika hafla hiyo fupi Dkt. Kimei pamoja na wafanyakazi waliohudhuria tukio hilo wamechangia papo kwa papo kiasi cha shilingi millioni tatu na nusu na kutoa wito makampuni,mabenki na taasisi nyingine kuchangia ili kufikia lengo la kampeni hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amesema CRDB imeonyesha Uzalendo kwa kuchangia ili kuboresha mazingira ya walimu kufanyakazi zao ambapo imekuwa taasisi ya kwanza ya kifedha kuunga Mkono kampeni hiyo.

Tazama Video hapa chini;

Comments

comments