Uhuru Media yafuturisha Wafanyakazi wake.

Kampuni ya Uhuru Media Group imefuturisha wafanyakazi wake kutoka kwenye kampuni zake tanzu ikiwamo Africa Media Group Ltd, inayomiliki vituo vya channel ten, Magic FM, DTV na CTN.

Akizungumza na wafanyakazi hao mara baada ya kufuturu, mwenyekiti mwenza wa Uhuru Media Group Dkt Abdullah Juma Saadallah… amewasisitizia wafanyakazi hao kuendeleza umoja na mshikamano kwani hiyo ndiyo nguzo kuu ya ufanisi wa kampuni yoyote ile yenye lengo la kwenda mbele zaidi.

Kwa upande wake Sheikh Sheikh Khamis Mtonga aliyemwakilisha Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salumu amewataka waandishi wa habari kote nchini kutumia vizuri kalami zao vizuri kwa manufaa ya Watanzania na nchi kwa ujumla.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Uhuru Media Group kwa ajili ya wafanyakazi wa kampuni zake zote tanzu, ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Comments

comments