Mawakili wa Upande wa Jamhuri kesi ya Mkurugenzi wa UDART wameiomba Mahakama ahirisho fupi.

Mawakili wa Upande wa Jamhuri katika kesi inayowakabili ya aliyekuwa Mkurugenzi wa UDART Robert Kisena na wenzake wameiomba Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ahirisho fupi kwa ajili ya kufanyia kazi maelezo ya mwendesha mashtaka wa serikali DPP huku wakidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya hakimu mkazi mkuu Thomas Simba, wakili wa serikali Wankyo Simon, amedai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamili hivyo wameiomba mahakama hiyo kesi hiyo itajwe tena tarehe 30 mwezi huu.

Kisena na wenzake hawakutokea mahakamani hapo ikidaiwa kuwa Kisena na mshtakiwa namba 4 ambao wanakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi ni wagonjwa.

Wakati huo huo kesi ya Florencia Membe ambaye ni mke wa Robert Kisena imeombewa ahirisho fupi kutokana na kusuburia hati ya mashtaka kutoka kwa mkurugenzi wa mashataka nchini DPP ambapo hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Augustine Lwizile amesema kutokana na ratiba yake kesi hiyo itatajwa tena tarehe 30 mwezi huu, ila kama uhitaji kutokana na kesi hiyo kuwa changa inaweza kusikilizwa na hakimu yeyote.

Mke wa Kisena anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na mumewe na wenzake watatu. Membe ni mkurugenzi wa kampuni ya Zenon oil gas limited ambapo anakabiliwa na mashtaka 7 likiwemo la kuisababishia hasara kampuni ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi ya UDART kiasi cha shilingi bilioni 2.4 ambapo amerudishwa tena rumande.
stand up

Comments

comments