Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka watendaji wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA katika wilaya yake kutumia lugha rafiki kwa walipa kodi wake na kuepuka kuwavuruga kwani si maadui wao.

Ametoa wito huo wakati akifungua mkutano wa Jukwaa la Wadau wa Kodi la Mkoa wa kodi Temeke, Jijini Dar es salaam, linalojumuisha wadau wa Biashara, uongozi wa TCCIA na TRA pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Amesema lengo la Jukwaa hilo ni kuboresha mahusiano kati ya wafanyabishara na mamlaka ya mapato Tanzania TRA, ikiwepo kubuni vyanzo vingine vya mapato na kuachana na hulka ya kutumia mabavu kwa walipa kodi.

Pamoja na hayo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amelitaka Jukwaa hilo kuwaorodhesha Wamachinga na kuwatambua ili kuwaingiza katika mazingira bora na kuanza kulipa kodi tofauti na sasa wanavyozidi kuwabana kwa njia zisizo rafiki.

Naye Meneja Mkoa wa Kodi Temeke Gamaliel Mafie amesema atazingatia maelekezo ya Mkuu huyo wa Wilaya na kutekeleza ili waeze kuongeza mapato zaidi pamoja na kuongeza mahusiano bora kwa walipa kodi.

Comments

comments