TFF imeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Uhlsport kwa ajili utengenezaji wa jezi zitakazotumiwa na timu ya taifa – ”Taifa Stars”

Shirikisho la soka nchini TFF limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Uhlsport kwa ajili utengenezaji wa jezi zitakazotumiwa na timu ya taifa ya Tanzania ”Taifa Stars” kuelekea mashindano ya mataifa ya Afrika AFCON mwaka huu nchini Misri.

Akizungumzia mkataba huo Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Wallace Karia, amesema jezi hizo zitazinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa kamati ya kusaidia Taifa Stars ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Mwakilishi wa Kampuni ya Romario Sport Minhaal Dewji ambao ndio watengenezaji wa jezi hizo amesema wameingia mkataba huo ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa kwa Taifa Stars huku akisisitiza kuwa jezi hizo zitakuwa katika ubora wa kiwango cha juu.

Comments

comments