TAKUKURU Yasisitiza Utaifishaji Mali Haramu.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Brigedia Jenerali JOHN MBUNGO, amesema serikali ya awamu ya tano itaendelea kutaifisha mali zinazopatikana kwa njia haramu ikiwemo ya RUSHWA kwa mujibu wa sheria ambapo hadi kufikia sasa zaidi ya shilingi Bilioni 14.7 zimerejeshwa serikalini pamoja na mali nyingine kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2019.

Naibu Brigedia Jenerali JOHN MBUNGO,amebainisha hayo katika kongamano la mapambano dhidi ya RUSHWA lililoandaliwa na mkoa wa Ruvuma kwa lengo kuhamasisha uzingatiaji wa maadili na haki za binadamu,ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza uongozi wa mkoa kwa kuandaa kongamano hilo na kutaka mikoa mingine kuiga mfano huo.

Hata hivyo kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Ruvuma YUSTINA CHAKANGA amesema kwa kipindi cha mwaka 2018 /2019 wameokoa zaidi ya shilingi milioni 47 zilizofanyiwa ubadhilifu pamoja na kupokea malalamiko 282 huku idara zinazoongozwa kwa malalamiko ni ardhi,serikali za mitaa, mahakama na jeshi polisi.

Katika kongamano hilo idara za serikali na binafsi walipata wasaa wa kujadili mada mbalimbali ikiwemo maadili ya utumishi wa umma na mgongano wa maslai huku kaulimbiu ikiwa “UADILIFU KATIKA JAMII NI NGUZO MUHIMU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA”.

Comments

comments