Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU imewaonya wananchi pamoja na watumishi wa Umma, na Serikali kujiepusha na Vitendo vya Rushwa, Utakatishaji fedha pamoja na Ufisadi kwani hivi sasa wana Mamlaka kamili ya Kutaifisha Mali za Watuhumiwa pindi Watakapothibitika wamejihusisha na Vitendo hivyo.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema kutokana na sheria hiyo wananchi na watumishi wa Umma na serikali wanatakiwa kuchukua tahadhari.

Kamishna Diwani amesema Takukuru kuanzia mwaka 2016-2019 imeingiza shilingi Billioni 14.9 kwa kutaifisha Mali za wala rushwa na Mafisadi, na imezuia mali nyingine zenye thamani shilingi billioni 20, nyumba 26, viwanja 47, magari 61 pamoja na mashamba 13 mali ambazo ni zao na rushwa na Ufisadi.

Katika hatua nyingine Takukuru imetangaza kumsaka Popote alipo Bi,Magreth Gonzaga ambaye anadaiwa kutoroka nje ya nchi kwa Makosa ya Utakatishaji fedha ambapo Takukuru imezuia Mali za mtuhumiwa ikiwemo Nyumba tatu za kifahari zilizopo kunduchi,viwanja vitatu vilivyopo kando ya bahari manispaa ya Temeke lakini pia Akaunti zake na magari.

Comments

comments