Sumu Kuvu yasababisha Vifo Manyara.

Watoto watatu wamefariki dunia wilayani Kiteto na wengine watano wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Dodoma baada ya kula chakula ukiwemo ugali ambao inadaiwa unga wake umeathirika na sumu kuvu ambayo inapatikana kwenye mazao yasiyokaushwa au kukauka vizuri.

Taarifa zinaleza kuwa watoto wawili wamepoteza maisha wakiwa katika hospitali ya wilaya ya Kiteto huku mmoja akipoteza maisha akiwa hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma walikolazwa watoto wengine watano walioathiriwa na sumu kuvu.

Hata hivyo tumezungumza na jamii za hapa kiteto kutaka kujua uelewa wao juu ya sumu kuvu.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa ameithibitishia channel ten juu ya matukio hayo ya vifo na watoto kulazwa.

Elimu ni jambo pekee na la muhimu linalohitajika kwa jamii kuiepusha kuendelea kuangamia kwa sumu kuvu ambayo jamii haina uelewa mpana juu ya kisababishi chake.

Comments

comments