Siku moja baada ya ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines kuua watu 157 kutoka zaidi mataifa 30, serikali ya Kenya imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja.

Raia 32 wa Kenya ni miongoni wa abiria wote 157 waliopoteza maisha kufuatia ajali hiyo ya ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya.

Ajali hiyo ilitokea mapema jana majira ya asubuhi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Bore Mjini Adis Ababa.

Taarifa ya awali ya kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines ilisema ndege hiyo ilibeba abiria kutoka mataifa 32 yakiwemo Marekani, Uingereza, China, India, Misri, Canada na Ufaransa

Jana Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kupitia ukurasa wake wa Twitter alitoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Katika hatua nyingine, Waziri wa usafirishaji wa Kenya, James machari amesema serikali ya nchi hiyo imepeleka maofisa kadhaa eneo la ajali na kuwataka raia kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.

Aidha shirika la ndege la Marekani la Boeing lililotengeneza ndege hiyo limeeleza kusikitishwa kwake na ajali hiyo iliyoua abiria wote na kuongeza kuwa litatoa msaada wa kiufundi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.


Comments

comments