Serikali kutumia Drones Kusambazia dawa kwenye maeneo magumu kufikika

26F35A5D00000578-0-image-a-25_1427211862103

Serikali inakusudia kutumia ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kusambaza dawa muhimu za binadamu kwenye vituo vya afya vya umma vilivyopo kwenye maeneo yenye changamoto ya kufikika kwa urahisi.

Mpango huo utakaoanza mwakani, utaanzia kwenye zahanati na vituo vya afya vya serikali elfu moja vilivyopo mkoani Dodoma kabla ya kusambazwa kwenye mikoa kumi iliyopo kanda ya ziwa, Nyanda za juu kusini na Pwani, ambapo wananchi zaidi ya milion kumi watanufaika na huduma hiyo.

Ndege zisizo na rubani – Drones zenye uwezo wa kubeba mzigo wa kilo moja na kusafiri umbali wa kilometa 150 kabla ya kumalizika betri yake zitatumika kusambaza dawa za chanjo, Dawa za matibabu ya kuumwa na Nyoka, Mbwa na kusafirishia Damu kwa ajili ya Matumizi ya vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali.

Makubaliano ya Utekelezaji wa Mpango huo yamesainiwa leo jiijini Dar es salaam baina ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na Watoto, Bohari ya Dawa MSD na watekelezaji wa mpango huo kampuni Zipline ya Marekani ambayo ndiyo itakayotoa ndege hizo na kusimamia uendeshaji wake.

Kupitia makubaliano hayo, Kampuni hiyo ya Kimarekani itatumia ndege zisizo na Rubani 120, ambapo gharama za huduma kwa sasa zitatolewa na wadau wa Maendeleo .

Comments

comments