Serikali kuwachukulia hatua wahujumu Uchumi.

Katika kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali zake, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeonya kuwachukulia hatua kali za kisheria, watu watakaothibitika kujihusisha na vitendo vya uhujumu uchumi, ikiwemoBiashara haramu ya utoroshaji wa madini nchini.

Serikali imetoa onyo hilo leo wakati ikikabidhiwa madini na mali nyingine, zilizotaifishwa kutokana na kesi ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2019, baada ya wafanyabiashara waliokuwa na madini hayo kukiri makosa yao.

Waziri wa Madini Dotto Biteko ametoa onyo hilo Jijini Mwanza, wakati mkurugenzi mkuu wa mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, alipokuwa akiikabidhi Wizara ya fedha na mipango mali zilizotaifishwa na Serikali, kutokana na kosa la utoroshaji wa Madini ya dhahabu.

Akiikabidhi wizara hiyo kilo 325 za madini hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 27, fedha taslimu shilingi milioni 305, magari mawili pamoja na mashine ya kupima ubora wa madini ya dhahabu, mkurugenzi mkuu wa mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga anasema.

Mali hizo zimetaifishwa na Serikali, baada ya kuhusishwa na biashara ya utoroshaji wa madini ya dhahabu kilo 319, iliyokamatwa Januari 4 mwaka huu wilayani Sengerema mkoani Mwanza ikiwa katika harakati za kutoroshwa, ikiwemo pia kilo tano za dhahabu zilizokamatwa baadaye.

Comments

comments