Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay mkoani Ruvuma.

Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay mkoani Ruvuma,reli ambayo inatarijiwa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa ukanda wa kusini kupitia sekta ya usafirishaji ambapo pamoja na usafirishaji wa bidhaa zingine chuma na makaa ya mawe yanatarajiwa kusafirishwa kwa wingi kupitia reli hiyo.

Hapa ni katika bandari ya Mtwara,upanuzi wa gati katika bandari hii unaendelea lengo likiwa ni kuifanya bandari hii kuweza kuhudumia meli kubwa na shehena kubwa ya mizigo.

Wakati ujenzi huo ukiwa unaendelea serikali inakusudia kujenga reli ya kisasa itakayoanzia katika bandari hiyo hadi Mambabay mkoani Ruvuma ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

Judith Nzamba ni mchumi kutoka shirika la reli nchini TRC anaeleza mikakati hiyo ambayo imefikia hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa wadau kutoka mikoa ya Mtwara na Ruvuma waliokutana kujadili mikakati hiyo.

Wakuu wa mikoa ya Mtwara na Ruvuma ambao ndiyo wameongoza majadiliano hayo wanasema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha fursa za uchumi zinafunguka kanda zote.

Comments

comments