Naibu waziri wa uchukuzi na mawasiliano amekiri kuwepo kwa mashambulizi mtandaoni

ethical-hackers-for-businesses-article

Naibu waziri wa uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amekiri kuwepo kwa mashambulizi mtandaoni dunia nzima ambayo mara tu yanapofanywa husambaa kwa kasi na kwa muda mfupi.

Hata hivyo amesema juhudi za pamoja zinahitajika katika kukabiliana na tatizo hilo ambalo huathiri sehemu muhimu ikiwemo mabenki na taasisi nyingine za kiserikali.

Akifungua mkutano wa kimataifa wa siku mbili unaojadili namna ya kabiliana na uhalifu mtandaoni Naibu waziri Nditiye amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia watumiaji wa mtandao wamekuwa wakiongezeka kwa kasi hali inayochochea kuongezeka kwa vitendo hivyo.

Aidha kupitia mkutano huo amewataka wataalamu wa masuala hayo kutumia fursa hiyo kuongeza ujuzi kwa kujifunza teknolojia mpya kutoka mataifa mengine pamoja na kuimarisha ushirikiano kwani tatizo hilo linapotokea ni lazima kushirikisha nchi nyingine.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya mawasiliano Tanzania – TCRA Mhandisi James Kilaba amesema Tanzania imekuwa ikichukua tahadhari kukabiliana na mashumbulizi mtandaoni kwa kujenga kituo maalumu kinachopokea taarifa za mashambulzi hayo lakini jambo la msingi ni kujenga na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma, kimiundombinu na kiufundi na kuendelea kuboresha vifaa kadri teknolojia inavyobadilika.

Comments

comments