Mwisho wa Mifuko ya Plastiki.

Kufuatia katazo la matumizi ya mifuko ya plasiki nchini wafanyabiashara mbalimbali mkoani Dodoma wameiomba serikali iongeze nguvu ya uzalishaji wa mifuko mbadala ili kukidhi mahitaji yaliyopo.

Rai hiyo imetolewa baada ya ziara iliyofanywa na ofisi ya makamu wa raisi kwa kushirikiana na ofisi ya mazingira ya jiji la Dodoma, iliyokuwa na lengo ilikuwa na lengo la kukagua maeneo mbalimbali ya jiji hilo, na kufanya tathimini ya utekelezaji wa agizo la serikali.

Awali akikagua soko la Majengo, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Raisi Prof William Mwegoa, amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuhamasisha wazalishaji wa mifuko mbadala ili waweze kukidhi mahitaji.

Comments

comments