Mwili wa Etienne Tshisekedi wawasili Kinshasa.

Mwili wa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa upinzani na Mmoja Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, umewasili jijini Kinshasa na wananchi leo wanatoa heshima zao za mwisho.

Mwili wa Tshisekedi uliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kinshasa usiku na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Serikali pamoja na wananchi waliokuwa nje ya uwanja kuusubiri mwili wake.

Tshisekedi alifariki akiwa mjini Brussels mwezi February mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 84, ambapo ameshindwa kushuhudia kuapishwa kwa mwanawe Felix Tshisekedi ambaye amekuwa Rais wa DRC kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Bw Felix aliahidi kuurejesha nyumbani mwili wa Baba yake na kuuzika katika eneo stahili, akitimiza ahadi ambayo alishindwa kuifanya wakati wa Utawala wa Rais Joseph Kabila.

Comments

comments