Msemaji wa shirika la ndege la Ethiopia amesema ndege zote za shirika hilo chapa Boeing 737 Max 8 hazitaruka kama hatua ya tahadhari, kufuatia ajali ya moja kati ya ndege zake iliyoua watu zaidi ya 157.

Bwana Asrat Begashaw amesema leo kwamba licha ya kwamba haijafahamika kile kilichosababisha ajali hiyo jana, shirika hilo limeamua kutorusha ndege zake nyingine chapa 737 Max 8 hadi taarifa nyingine itakapotolewa, ikiwa ni kuchukua tahadhari zaidi.

Mamlala ya safari za anga nchini China pia imeamuru mashirika yote ya ndege nchini humo yasirushe ndege zake za Boeing 737 Max 8 kuanzia leo baada ya ajali ya shirika la ndege la Ethiopia.

Nae mkuu wa shirika la taifa la usalama wa usafirishaji nchini Indonesia Soerjanto Thahjono, ametoa ombi la kusaidia uchunguzi katika ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia iliyotokea jana.

Comments

comments