Makampuni ya simu za mkononi, Yapewa changamoto kupanua wigo wa huduma

Africa-internet-access-with-mobile-phones

Makampuni ya simu za mikononi kwa kushirikiana na serikali pamoja na sekta binafsi yametakiwa kuhakikisha mawasiliano ya simu za mkononi yanamfikia kila mtu vijijini na mijini ili kusaidia litakalosaidia katika kutekeleza na kufikiwa kwa malengo endelevu 17 yaliyowekwa na dunia (.SDGs).

Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati ambapo amesema asilimia 60 ya watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini na 57 kati yao wameachwa nje ya mtandao wa matumizi ya simu za mkononi hivyo kuwanyima fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia mitandao ya simu ikiwemo za kiuchumi, afya, elimu na mabadiliko ya teknolojia hususan ya kidigit.

Akifungua mkutano wa mwaka 2017 ujulinao GSMA MOBILE 360 uliowakutanisha waendeshaji wa mitandao ya simu, wataalam wabunifu na serikali Makamu wa Rais amesema licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo bado kuna changamoto zinazozikabili nchi nyingi za Afrika katika kufikia malengo endelevu ikiwemo vikwazo vya kibajeti, ubovu wa miundombinu na upungufu wa rasilimali watu ambazo zinachangia kushibdwa kwa sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa GSMA Dk. Mats Granryd akizungumzia matarajio ya GSMA amesema ni kuwaunganisha vijana na kuziba pengo la kijinsia pamoja na kuunganisha shehemu mbalimbali hata zile ambazo fursa zake za kisoko bado zipo chini kama vile DRC Congo, Ethiopia, Nigeria na Tanzania ambazo kwa pamoja watakamilisha idadi ya watumiaji wapya wa simu za mkononi wapatao milioni 115 chini ya jangwa la sahara ifikapo mwaka 2020 pamoja na kundi la watoto wenye umri wa mika 16 na wanawake waliosahaulika.

Comments

comments