Ligi Kuu Uingereza – EPL: Chelsea mabingwa 2017, Conte ataka wabebe na kombe la FA

7

Chelsea waliibuka mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) huku wakibakiza Mechi 2 kwa kuifunga West Bromwich Albion 1-0 huko the Hawthorns kwa bao la dakika ya 82 la Michy Batshuayi.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte ameitaka timu hiyo kugeuza msimu huu kuwa war aha kwa kuwataka kubeba pia kombe la FA. Conte, ambae alijiunga na Chelsea mwanzoni mwa msimu baada ya kuiacha timu ya Taifa ya Italy mara baada ya fainali za EURO 2016, amesema kubadili mfumo na kutumia difensi ya watu 3 mwezi Septemba mara baada ya kupigwa 3-0 na Arsenal kuliwazindua na kupigania Ubingwa.

Mei 27 huko Wembley Jijini London, Chelsea wataivaa Arsenal katika Fainali ya FA CUP.

Nayo Crystal Palace imejihakikishia kubaki katika ligi hiyo baada ya kuichapa Hull City goli 4-0. Nayo Liverpool imejihakikishia uwezo wa kubaki 4 bora kwa kuitwanga West Ham United mabao 4-0. Manchester United imepoteza mchezo wake dhidi ya Tottenham Hotspur kwa kukubali kichapo cha 2-1. Ligi hiyo inaendelea leo kwa mchezo kati ya Mabingwa Chelsea watakapokutana na Watford.

Comments

comments