Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido amerejea leo nchini humo, baada ya ziara katika mataifa ya Amerika, na kushinikiza maandamano zaidi dhidi ya rais Nicolas Maduro.

Guaido ambaye alijiapisha kuwa rais wa watu na kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani, amepokelewa na maelfu ya wafuasi wake jijini Caracas.

Kiongozi huyo amerejea nyumbani licha ya wasiwasi kuwa angekamatwa, baada ya kukiuka masharti ya Mahakama ya Juu, iliyokuwa imemzuia kutoka nje ya nchi hiyo.

Hata hivyo Marekani imeionya serikali ya Rais Nicolas Maduro nchini Venezuela kutochukua hatua yoyote dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani, huku Guaido mwenyewe amewatolea mwito wafuasi wake kuendelea kuandamana kwa wingi kwa lengo la kumshinikiza Rais Maduro kujiuzulu.

Marekani na nchi kiasi 50 nyingine zinamtambua Guaido kama Rais halali wa Venezuela huku Maduro akisema analengwa katika njama ya mapinduzi inayoungwa mkono na Marekani.

Comments

comments