Kikao Kazi cha Maelekezo kwa Watendaji CCM Mwanza.

Wakati joto la uchaguzi wa serikali za mitaa nchini likipanda, Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza, kimewataka watendaji wa kata kusimamia vyema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ili kuwawezesha wapiga kura kutambua vituo vyao.

Katibu wa Chama hicho mkoa wa Mwanza Salum Kalii, ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya (CCM) mkoani hapa, katika kikao kazi cha maelekezo kwa watendaji wa kata kinacholenga kuboresha daftari hilo.

Katika kikao hicho amesema agizo hilo, litasaidia kudhibiti mazingira yaliyokuwa yakichangia kuwepo na hujuma za opotevu wa kura, kama ilivyotokea kwenye baadhi ya chaguzi zilizopita nchini.

Simon Mangelepa ni katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza, anatumia kikao hicho kuwashauri wanachama wa chama hicho kuwa na umoja na mshikamano, ili kukijengea ushindi chama hicho.

Kutokana na maelekezo hayo baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakaeleza jinsi walivyopokea ushauri huo na kuahidi kuyafanyia kazi, ili kukipa ushindi wa asilimia mia moja Chama cha Mapinduzi (CCM).

Sekretarieti ya Chama cha Mapinuzi (CCM) mkoa wa Mwanza hukutana kila mwaka, ili kujadili masuala mbalimbali, yanayolenga kuboresha ufanisi wa chama katika chaguzi, lakini pia kujadili mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Comments

comments