Katibu Mkuu CCM Dkt. Bashiru Ally leo amekutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Frelimo (Veterans) nchini Msumbiji .

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally leo amekutana na Kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Frelimo (Veterans) nchini Msumbiji katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Channel Ten Dkt, Bashiru Ally amesema Ujumbe huo ambao upo nchini kwa ziara ya siku tatu pamoja na mambo mengine utatembelea ujenzi wa chuo cha uongozi cha Umma Kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani ambacho kinajengwa kwa ushirikiano wa nchi sita.

Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha wapigania uhuru wa Frelimo (veterans) Faustino Fernando ameishukuru serikali ya Tanzania kwa Ushirikiano wa Kihistoria ambao ulisaidia nchi zilizopo kusini mwa Afrika kupata uhuru ikiwemo Msumbiji, pamoja na misaada ya kibinadamu ya dawa na chakula baada ya nchi hiyo kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na kimbunga ambapo mamia ya wananchi wa Msumbiji walipoteza maisha na wengine kupoteza makazi.

Ujumbe huo umemhusisha pia mjumbe wa Kamati Kuu ya Frelimo Helena Musikan pamoja na balozi wa Msumbiji hapa nchini Monica Patricio Clemento Mussa.

Comments

comments