Kampuni ya Africa Media Group wamiliki wa Kituo cha Television cha Channel Ten na Radio Magic Fm imezindua nembo ya maonesho ya Taasisi za kifedha na Bima (Banking Finance and Insurance Expo 2019).

Kampuni ya Africa Media Group wamiliki wa Kituo cha Television cha Channel Ten na Radio Magic Fm imezindua nembo ya maonesho ya Taasisi za kifedha na Bima (Banking Finance and Insurance Expo 2019) yenye lengo la kutaka kufahamisha wananchi hasa wa Dodoma nini taasisi hizo zinafanya sambamba na kujua fursa zilizopo katika Taasisi hizo na kuzitumia.

Akizungumza mara baada ya kuzindua nembo hiyo jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Africa Media Group Jaffary Haniu amesema lengo la maonesho hayo ni kupeleka fursa za Taasisi za kifedha jijini Dodoma ambako ndio Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM na Serikali na kuhamasisha wananchi wa Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali zitolewazo na Taasisi za kifedha na Bima ikiwemo Mikopo itakayowapatia mitaji ya biashara.

Comments

comments