Ofisi ya Msitu wa Mbizi uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeanza mikakati ya kupambana na moto kichaa

Ofisi ya Msitu wa Mbizi uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeanza mikakati ya kupambana na moto kichaa unaotokea kila mwaka na kuharibu miti iliyopo katika shamba hilo licha ya kuwa msitu huo una vyanzo vya maji yanayotumika katika mji wa Sumbawanga kwa kuwakutanisha wakazi wa vijiji kumi na moja vinavyopakana na msitu wa Mbizi na kuwapa mafunzo ya kudhibiti moto pori unaochangia uharibifu wa ustawi wa msitu huo.

Baadhi ya viongozi kutoka vijiji kumi na moja vinavyouzunguka msitu wa mbizi wakielezea njia sahihi za kuutunza msitu huo ambao ni chanzo kikuu cha hifadhi ya maji kwa ajili ya wakazi wa mji wa Sumbawanga.

Meneja wa msitu huo Mohamed Kiangi amesema zaidi ya miche milioni mbili iliyopandwa katika shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita inakabiliwa na hatari ya kutekekea kwa moto kutokana na shughuli za kibinadamu

Mafunzo hayo ya siku moja kwa viongozi wa vijiji hivyo kumi na moja yamefunguliwa na mkuu wa Jeshi la polisi wilaya ya Sumbawanga, Chacha Maro ambaye amesema vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kusimamia sheria za udhibiti wa hifadhi ya misitu ili kulinda uharibifu wa mazingira

Msitu wa Mbizi umekuwa ukipatwa na janga la kuunguzwa moto na baadhi ya wananchi wanaovamia msitu huo kwa lengo la kuwinda wanyama, panya na hata kulima pembezoni mwa msitu huo.

Comments

comments