Teknolojia na huduma za simu zimeliingizia Bara la Afrika mapato

A Kinshasa resident makes a cell phone call in Kinshasa, Congo, November 10, 2006. Africa is currently the fastest-growing market for cell phone contracts in the world. (Benedicte Kurzen/Chicago Tribune/MCT)

Imeelezwa kuwa teknolojia na huduma za simu zimeliingizia Bara la Afrika mapato ya ndani kwa asilimia 6.7 kwa mwaka 2015 dola za kimarekani bilioni 150 kwa thamani ya kiuchumi ambapo mapato hayo yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 210 ikiwa ni sawa na asilimia 7.6 kwenye pato la ndani la Taifa.

Hayo yameelezwa na Meneja uhusiano wa Tasisi ya Jumia Travel, Geofrey Kijanga kwenye hafla ya kampeni yenye lengo la kuwarahisishia watanzania kupata fulsa za safari za kitalii ndani na nje ya nchi ambapo amesema kampeni hiyo inamrahisishia mteja kuweza kupata huduma za safari, kupitia huduma ya intaneti ambayo inapatikana kwenye mtandano wa Taasisi hiyo.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka kwenye moja ya hotel ambazo zinashirikiana na Taasisi hiyo Mganja Suleiman amesema kupitia huduma hiyo ya upatikana wa huduma za safari za kitaliii imesadia kwa kiasi kikubwa kuongezeaka kwa wateja kwenye Hotel yake.

Taasisi ya Jumia Travel imekuwa ikijushughulisha na kutoa huduma za usafiri kwa watalii na wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi ambapo kwa sasa Taasisi hiyo inafanya Kampeni hiyo lengo likiwa kuwaelimihsa watanzania kutumia huduma zake.

Comments

comments