Dodoma yadhamiria Asilimia 100 ya Uandikishaji CHF.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. BINILITH MAHENGE amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kufanya oparesheni kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya CHF iliyoboresha ili kufikia malengo ya asilimia mia moja.

Dkt. Mahenge ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na taarifa iliyotolewa na mratibu wa CHF mkoa ikionyesha kiwango kidogo cha watu waliojiandikisha katika mfuko huo.

Agizo hilo limetolewa katika uzinduzi na ugawaji wa vitambulisho vya bima ya afya kupitia kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ya CHF kwa gharama ya shilingi elfu 30 kila familia wilayani Chamwino.

Ambapo taarifa ya mratibu wa CHF mkoa Dkt. FRANSIC LUTALALA ikaonyesha bado idadi ya wananchi waliojiunga na mfuko huo ni ndogo.

Kufuatia taarifa hiyo kutomridhisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge anaanza kwa kuagiza wakuu wa wilaya kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko huo.

Kasha akataka ifanyike oparesheni maalumu itakayowahisisha viongozi wote wa wilaya, huku baadhi ya wananchi waliojiunga na mfuko huo wakieleza manufaa yake.

Comments

comments