Screen Shot 2017-01-16 at 4.39.33 PM

Serikali yasema hakuna njaa nchini Tathimini ya hali ya chakula katika Halmashauri 55 yaendelea

Serikali imesema hakuna njaa nchini, na kwa sasa hali ya chakula inaridhisha licha ya eneo kubwa la nchi kukosa mvua za msimu wa vuli ambazo zimesababisha ukame kwa baadhi ya maeneo. Kwa sasa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Shirika la Chakula Duniani, Taasisi ya Chakula na[…]

screen-shot-2017-01-07-at-6-15-29-pm

Tishio la Njaa Kwimba, Wananchi wawasilisha kilio serikalini

Wakati tishio la njaa likiendelea kutikisa katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na ukame, wakazi wa Kijiji cha Manawa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, wamelazimika kuzuia msafara wa mkuu wa mkoa huo John Mongela, ili kuwasilisha kilio cha njaa inayowakabili. Kutokana na kilio hicho kilichosababishwa na ukosefu wa Mvua, wakazi hao wamelazimika kubeba mabua ya Mahindi yaliyokauka,[…]

putin

Vladmiri Putin Aliamuru udukuzi dhidi ya Hillary Clinton

Urusi imepinga shutuma kuwa Rais wa nchi hiyo Vladmir Putin,aliamuru ufanyike udukuzi,dhidi ya Hillary Clinton na Chama chake cha Democratic,kumsaidia Donald Trump,kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Andrey Klimov,ambaye ni makamu mwenyekiti wa Seneti inayoshughulika na uhusiano wa kimataifa,amesema,Urusi ni tishio na imekuwa ikisakamwa kwa maneno mabaya huku Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Klemlin,ikifananishwa[…]

img_20160418_114236

Tabia ya wizi imeibuka mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam

Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wameomba waendesha mradi UDA-RT kuimarisha ulinzi katika vituo vya mabasi hayo kutokana na kuibuka kwa tabia ya wizi katika vituo hivyo jambo ambalo hapo awali halikuwepo. Wakizungumza na Channel Ten abiria hao wamesema wanadhani tatizo hilo limeibuka katika kipindi hiki kutokana na kusitishwa kwa[…]

a1

Rais Magufuli, leo amemuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo amemuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera. Hafla ya kuapishwa kwa Kamishna Diwani Athuman Msuya imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman, Waziri wa[…]

Hospitali ya Ocean Road

Jamii Yakumbushwa Mazoea ya Kuwatembelea na Kuwajulia Hali Wagonjwa

  Hayo yamebainishwa na mchungaji wa kanisa la KKKT Herman Kiporoza aliyeambatana na kwaya kuu ya kanisa hilo kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza nyingi ya faida za kuwatembelea wagonjwa mahospitalini. Wakiwa Ocean Road, mchungaji Kiporoza na kwaya hiyo walianza[…]

g1

Mkuu wa Mkoa wa Arusha M.Gambo Aagiza Hati ya Umiliki Ranch ya Manyara Kurudi kwa Halmashauri

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameuelekeza uongozi wa halamashauri ya wilaya ya Monduli, waendeshaji wa shamba la mifugo la Manyara ranch, AWF na bodi ya wadhamini ya uendeshaji wa shamba hilo TLCT kuanza mara moja mchakato rasmi wa kuhakikisha hati ya umiliki wa shamba hilo inarudishwa kwa halmashauri tofauti na ilivyo sasa ambapo[…]