Serikali kununua Rada nne kuwezesha kuona aina yoyote ya ndege inayoingia ama kupita katika anga la Tanzania

Serikali imesema itanunua rada nne ambazo zitawekwa sehemu mbali mbali za Tanzania ili kuwezesha kuona aina yoyote ya ndege inayoingia ama kupita katika anga la Tanzania ili kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa salama mda wote. Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Professor Makae Mbalawa ambae ametembelea uwanja wa[…]

TTCL yaibuka na kasi Mpya ya 4G LTE Morogoro

Serikali imedhamiria kuwachukulia hatua kali watu wataohusika katika uharibifu na kuhujumu miundo mbinu ya kampuni ya simu Tanzania TTCL mtandao ambao licha ya kutegemewa na wananchi kwa asilimia kubwa bado ni chachu ya maendeleo na katika kuchangia pato la taifa. Akiongea katika uzinduzi wa huduma za 4G LTE ya kampuni ya simu Tanzania mkoani Morogoro[…]

Wino bandia wa Komputa uliokamatwa DAR Wadau wa Maduka ya Vifaa vya Ofisi watoa maoni

Siku moja bada ya Tume ya ushindani, FCC,kukamata shehena ya kontena kumi za wino bandia unaotumika kwenye kompyuta Tona,zenye thamani ya shilingi bilioni nane hadi tisa,zinazoingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waminifu wa China,baadhi ya wafanyakazi katika maduka ya vifaa vya ofisi ,jijini Dar es Salaam,wamezungumzia kadhia hiyo iliyopatikana mtaa wa Senegal,Upanga,jijini humo.   Tume ya[…]

Baadhi ya wakazi Mwanza wameiomba Serikali kufanya marekebisho kwa kupunguza gharama zinazotozwa na Kampuni ya simu

Baadhi ya wakazi mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kufanya marekebisho kwa kupunguza gharama zinazotozwa na Kampuni ya mitandao ya simu nchini, ili kuwawezesha Wananchi wengi kumudu gharama hizo pamoja na kunufaika na mawasiliano hayo kijamii na kiuchumi. Viwango vya gharama vinazotozwa na mitandao ya simu nchini, vinatajwa na Wananchi kuwa ni aghari, ambapo licha ya kuiomba[…]

Huduma za mawasiliano vijijini Wasiofika maeneo waliyoomba leseni kunyang’anywa

Serikali imetishia kuzinyang’anya leseni za masafa kampuni za huduma za mawasiliano nchini zilizopewa ruzuku ya kutekeleza miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini lakini yameshindwa kukamilisha miradi hiyo. Serikali kupitia mfuko wa Mawasiliano kwa wote, imekuwa ikitoa ruzuku ya fedha za ujenzi wa minara ya mawasiliano kwenye kata 443 zilizopo maeneo ya vijijini ili kufikisha[…]

DIT imebuni mifumo ya TEHAMA na kutengeneza vifaa vya kuchukulia na kupimia Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam – DIT, imebuni mifumo ya TEHAMA na kutengeneza vifaa vya kuchukulia na kupimia Mabadiliko ya Hali ya Hewa¬† ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa taarifa hizo kwa walengwa. Kubuniwa kwa vifaa na mifumo hiyo kutasaidia kuongeza ufanisi kwa mamlaka ya hali ya hewa[…]

Taasisi 72 za Serikali zaunganishwa kwenye Mtandao

Serikali imeunganisha Taasisi 72 katika Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali kupitia Mkongo wa Taifa hatua ambayo kwa kiasi kikubwa itapunguza gharama za mawasiliano Serikalini, ikiwa ni pamoja na kuzisaidia Taasisi za Serikali kuwa na Mawasiliano bora ya Kielektroniki, hivyo kuboresha utendaji kazi na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma. Akizungumza na Waandishi wa Habari[…]