Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kambi ya wachezaji wa timu ya Taifa na kuwaeleza kwamba Serikali na wananchi wana matumaini makubwa kwa timu yao, hivyo wahakikishe wanapata ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda leo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amewaeleza wachezaji hao kuwa Serikali ina imani nao na kwamba wasiwe na wasiwasi kwa sababu hawana tofauti yoyote na wachezaji wa timu nyingine duniani, hivyo akawataka wakapigane kufa na kupona ili kupata ushindi na hatimaye kufuzu. Taifa Stars kupitia Nahodha wake Mbwana Samata wamemwahidi Waziri Mkuu kwamba watapigana kufa na kupona kuhakikisha kwamba[…]

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo inaendesha Kampeni ya kutoa elimu nchi nzima kwa vijana ili vijana hao waweze kukuza vipaji vyao pamoja na kuwa na weledi katika utengenezaji wa picha za filamu.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo katika Mji mdogo wa Nduguti,wilayani Mkalama baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo iliyoonyesha jitihada za kulikarabati jengo la Boma la Mjerumani na kubaini pia kuwa wilaya ya Mkalala bado ipo nyuma katika masuala ya utengenezaji wa picha za filamu na ndipo akatoa ahadi kwa wana – Mkalama. Aidha Dkt. Mwakyembe[…]

Kamati ya Saa 72 inayosimamia Ligi Kuu Tanzania Bara yailima faini ya milioni Sita Yanga pamoja na Kutoa Onyo kali kwa Makocha wa Vilabu Vinavyoshiriki Ligi Kuu Bara kwa utovu wa Nidhamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amewataka makocha ambao wanashambulia waamuzi wapeleke ushahidi ndani ya shirikisho la soka TFF kwaajili ya hatua zichukuliwe na vyombo vinavyoongoza shirikisho hilo. Aidha Wambura ameainisha adhabu kwa timu za Simba,Yanga na Azam Fc ambazo zilikiuka utaratibu wa kisheria kwa kutotumia milango rasmi[…]

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka.

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka na hivyo kuchochea maendeleo ya kijami na kiuchumi. Channel Ten imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam ambao wamesema, kutokana na kukua kwa[…]

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ngazi ya klabu, Timu ya Simba ya DSM leo watakuwa Uwanja wa Taifa wakitafuta pointi muhimu mbele ya timu ya Al Ahly ya Misri.

Mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni wa mzunguko wa nne na mpaka sasa hakuna timu ambayo ina uhakika wa kwenda robo fainali kwenye kundi lao la D. Simba ipo Kundi D ikiwa na timu za Al Ahly iliyo kileleni na pointi saba, AS Vita ya CONGO DRC yenyewe ni[…]

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini DSM ikiwemo utakatishaji fedha wa Mil.75.

Katika kesi hiyo Wambura anakabiliwa na shtaka moja la kughushi, Shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha. Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali George Barasa akisaidiana na Moza Kasubi pamoja na Imani Mitumezizi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin[…]

Shirika la Reli Tanzania limesema kuwa milango bado ipo wazi kwa makundi mbalimbali kuutembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR inayojengwa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa lengo la kujifunza kama walivyofanya wasanii mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kungu Kadogosa mara baada ya kupokea wasanii,wanamichezo na washereheshaji zaidi ya 300 waliotembela mradi wam Ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa. Wasanii hao walitumia usafiri wa treni ya delux na kushuhudia ujenzi wa Reli hiyo wakiwa ndani ya treni hiyo ambapo pia walikuwa wakishuka na kujionea[…]