Baraza la sanaa la Taifa BASATA limewataka wasanii kote nchini kuzitambua haki zinazopatikana kwenye kazi wanazozifanya.

Baraza la sanaa la Taifa BASATA limewataka wasanii kote nchini kuzitambua haki zinazopatikana kwenye kazi wanazozifanya ili ziweze kuwaletea maendeleo, lakini pia ziweze kulinufaisha taifa kiuchumi. Rai hiyo imetolewa imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya BASATA Habby Gunze wakati wa kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa sanaa pamoja na viongozi wa bodi hiyo kwa lengo la[…]

UMISETA: matokeo ya ligi ya Soka ya Wanawake.

Wanafunzi wa kike wanaocheza mpira wa miguu katika michuano ya umiseta mkoani Mtwara wameshauri viongozi wa shirikisho la soka nchini TFF kuweka mkazo kwenye ligi ya soka la wanawake ngazi ya chini itakayowezesha kuibua vipaji vya wanawake watakaoweza kuchezea timu ya taifa ya soka la wanawake. Ni michuano ya umiseta ikiendelea hapa mkoani Mtwara na[…]

Mashidano ya wazi wa TANAPA Gofu yaanza Lugalo.

Mashindano ya wazi ya Gofu yaliyodhaminiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA yameanza leo katika viwanja vya klabu ya Gofu Lugalo, yakishirikisha takriban wachezaji themanini kutoka ndani na nje ya nchi. TANAPA LUGALO OPEN ni miongoni mwa mashindano makubwa yaliyo kwenye lakenda ya Chama cha Gofu Tanzania TGU, yakishirikisha idadi kubwa ya wachezaji kutoka[…]

Wabunge watoa angalizo Afya za Wanamichezo.

Serikali imeliarifu bunge kuwa itapokea wazo ikiona inafaa kupeleka muswada wa sheria Bungeni ya kuwalazimisha wanamichezo kupima afya zao licha ya kuwepo kwa sera ya huduma za afya kwa wanamichezo nchini ambayo haitekelezwi ipasavyo, ili kuepuka vifo vinavyotokea viwanjani. Naibu waziri wa wizara ya habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, JULIANA SHONZA, ametoa kauli hiyo bungeni,[…]

TFF imeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Uhlsport kwa ajili utengenezaji wa jezi zitakazotumiwa na timu ya taifa – ”Taifa Stars”

Shirikisho la soka nchini TFF limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Uhlsport kwa ajili utengenezaji wa jezi zitakazotumiwa na timu ya taifa ya Tanzania ”Taifa Stars” kuelekea mashindano ya mataifa ya Afrika AFCON mwaka huu nchini Misri. Akizungumzia mkataba huo Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Wallace Karia, amesema jezi hizo[…]

Udhamini wa Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao 2019/2020.

Benki ya NMB ipo kwenye mazungumzo na shirikisho la mpira nchini (TFF), ili benki hiyo iwe mdhamini mkuu wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu ujao. Hayo yamewekwa bayana na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA, katika hafla futari iliyoandaliwa na benki ya NMB, jijini Dodoma. Aidha, Waziri Mkuu alichukua wasaa huo kuipongeza na kuishukuru benki[…]