Mapambano dhidi ya dawa za kulevya Mkuu wa Wilaya ya Muheza aomba ushirikiano kwa wananchi

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuwafichua wanaojihusisha na uuzaji usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya. Wito huo ameutoa wakati akihutubia wananchi wa katika hafla ya uzinduzi wa visima viwili vya maji katika kata ya Bwembwera na kijiji cha kwakifua wilayani muheza .[…]

Mahakama Kuu kanda ya DSM leo imetoa zuio la kutomkamata au kuwekwa kizuizini Freeman Mbowe

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam leo imetoa zuio la kutomkamata Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Freeman Mbowe mpaka maombi aliyowasilisha ya kuomba kutokukamatwa na kuwekwa kizuizini yatakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. Zuio hilo limetolewa na jopo la majaji mahakamani hapo ambapo maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na[…]

Ugonjwa wa Ndiganakali Wafugaji kanda ya ziwa kuchanja dawa

Kutokana na ugonjwa wa Ndiganakali kubainika kuteketeza karibia asilimia 70 mpaka 80 ya Ndama katika maeneo mbalimbali nchini, wafugaji kanda ya ziwa wameshauriwa kuwachanja ndama wao chanjo maalumu ya Ndiagana kali ili kuwaepusha na vifo na gharama kubwa ya kutibu ngíombe hao pale wanapopata ugonjwa huo unaosababishwa na kupe. Kwa mujibu wa jopo la wataalamu[…]

Barabara za Lami kuufungua Mkoa wa Manyara Serikali yapanga kujenga barabara mbili kuu za lami

SERIKALI imepanga kujenga barabara mbili kuu za lami ambazo zikikamilika zitasaidia kuunganisha mikoa mitano ya Arusha, Singida, Simiyu, Shinyanga na Manyara. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Haydom na Mbulu Mjini kwenye mikutano wa hadhara iliyofanyika wilayani Mbulu, mkoani Manyara. Amezitaja barabara hizo kuwa[…]