13 wauawa katika shambulizi nchini Marekani.

Mtandao wa Marekani wa Gun Violence Archive umeonyesha kuwa shambulizi la kutumia silaha lililotokea katika fukwe za mapumziko mjini Virginia Marekani jana ni la 150 kufanyika kwa mwaka 2019 ambapo limesababisha vifo vya takriban watu kumi na watau tatu na wengine sita kujeruhiwa katika shambulizi la risasi lililotokea katika jengo la serikali. Mtandao huo umeripoti[…]

Hoja ya kulivunja Bunge Israel .

Israel italazimika kufanya uchaguzi mpya mnamo mwezi Septemba mwaka huu, baada ya wabunge kupitisha hoja ya kulivunja bunge kufuatia Waziri mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya muungano leo. Bunge la Knesset limeidhinisha kura ya awali ya kuvunjwa kwake na kuifanya nchi hiyo kuingia katika uchaguzi wa pili wa mapema mwaka huu. Wabunge walipiga kura[…]

Chama Cha Front Nationale kinachoongozwa na Mwanamama Marine Le Pen kinaongoza katika nafasi ya kwanza kwenye Uchaguzi wa umoja wa Ulaya .

Chama Cha Front Nationale kinachoongozwa na Mwanamama Marine Le Pen kinaongoza katika nafasi ya kwanza kwenye Uchaguzi wa umoja wa Ulaya nchini Ufaransa, matokeo ambayo ni pigo kwa Utawala wa rais Emmanuel Macron anayetetea umoja wa Ulaya. Chama cha Le Pen National Rally kimepata Asilimia 23.31ya kura zote huku Chama cha mrengo wa kati cha[…]

Wagombea wanaowania kumrithi Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May wajiandaa kuanza kampeni leo.

Wagombea wanaowania kumrithi Theresa May kama Waziri Mkuu wa Uingereza wanajiandaa kuanza Kampeni leo,na kuacha mchakato wa kujiondoa Umoja wa Ulaya-Brexit ukiwa mashakani. May alitangaza kujiuzulu wadhifa wake jana na kusababisha kuanza kwa kinyang’anyiro cha kumsaka mrithi wake ndani ya kipindi cha miezi miwili. May atajiuzulu kama Kiongozi wa Chama Cha Conservative Juni 7 lakini[…]

Serikali ya Ujerumani imeamua kuzuia Euro Milioni 100 ilizoahidi kuipa Serikali ya Uganda.

Serikali ya Ujerumani imeamua kuzuia Euro Milioni 100 ilizoahidi kuipa Serikali ya Uganda kwa ajili ya kuwapa makazi wakimbizi. Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa mpango wa Wakimbizi wa Uganda mnamo mwaka wa 2018 uligundua ushahidi wa ufisadi. Kashfa hiyo ilijitokeza baada ya mvujishaji ndani ya Serikali ya Uganda kuwafahamisha wafadhili kuwa kiasi kikubwa cha[…]

Viongozi wa Upinzani Nchini Sudan waitisha mgomo mkubwa wa siku mbili.

Viongozi wa Upinzani Nchini Sudan wameitisha mgomo mkubwa wa siku mbili kwa ajili ya kulishinikiza zaidi Baraza la Kijeshi la Mpito kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. Kwa mujibu wa Chama Cha Wanataaluma wa nchini Sudan wameeleza kuwa Mgomo huo umepangwa kuanza Wiki ijayo siku ya Jumanne na kufuatiwa na Maandamano ya nchi nzima siku[…]

Mzinduzi wa Kampuni ya Huawei asema suala la msingi la biashara kati ya China na Marekani ni kiwango cha elimu.

Mzinduzi wa Kampuni ya Huawei ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Ren Zhengfei amesema, elimu ya msingi na ya ufundi vinatakiwa kufuatiliwa zaidi, na suala la msingi la biashara kati ya China na Marekani ni kiwango cha elimu. Bw. Ren alipohojiwa na kituo kikuu cha redio na televisheni cha China CMG[…]