Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani achaguliwa kuwa Rais wa Halmashauri kuu Tume ya Ulaya .

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ,Ursula Von der Leyen, amechaguliwa Mkuu wa Tume ya Ulaya huku Bunge hilo likithibitisha uteuzi wake na hivo kuwa Mwanamke wa kwanza kuongoza taasisi Kuu ya Umoja wa Ulaya. Uthibitishwaji huo ulihitaji wingi wa kura 374 na Waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani anayendoka alipita kwa ziada ya kura tisa.[…]

Mtu mmoja amefariki Dunia na mamia ya Nyumba kuharibiwa baada ya tetemeko kubwa la Ardhi

Mtu mmoja amefariki dunia na mamia ya nyumba kuharibiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga Mashariki mwa Indonesia, kwa mujibu wa ripoti ya awali. Tetemeko hilo la ardhi lilitokea muda mfupi baada ya saa 12:00 jioni Kaskazini mwa Rasi ya Maluku, kwenye kina cha kilomita 10, na kusababisha hofu kwa wakazi na kulazimika kuyahama[…]

Rais wa China XI Jimping na Viongozi wa wengine wa Dunia wanakutana Osaka- Japan.

Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wa Dunia wanakutana katika mji wa Osaka huko Japan kwa mkutano wa kilele wa nchi ishirini zenye uchumi mkubwa duniani yaani G20. Mkutano huo unatarajiwa kufunikwa na mizozo ya biashara na siasa za kikanda. Rais Donald Trump alitarajiwa kuwasili baadae leo na anatarajiwa kukutana na Bw. Xi[…]

Mbio za kuwania uteuzi wa chama cha Democratic – Marekani zimeshika kasi.

Mbio za kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa mwakani nchini Marekani zimeshika kasi, ambapo wagombea 10 kati ya ishirini wameshindana katika mdahalo wa televisheni. Wagombea 10 kati ya 20 wamechuana usiku wa kuamkia leo katika mdahalo wa televisheni ambao ulitazamwa na mamilioni ya raia wa Marekai ambao watapima ikiwa[…]

Waziri Mkuu wa Italia asiye na chama Guiseppe Conte, ametishia kujiuzulu.

Waziri Mkuu wa Italia asiye na chama Guiseppe Conte, ametishia kujiuzulu kutokana na mzozo unaoendelea kati ya vyama washirika katika serikali. Wakati huo huo ameutaka Muungano wa vyama tawala vya siasa kali za Mlengo wa kulia na kile cha kizalendo kuwajibika. Conte amesema mjini Rome kuwa ataachia nafasi hiyo endapo vyama vya League na Vuguvugu[…]

Wanajeshi wa Sudan watumia nguvu.

Wanajeshi nchini Sudan wametumia nguvu kuvunja kambi ya waandamanaji mapema leo nje ya makao makuu yao jijini Khartoum, baada ya mazungmzo na viongozi wa waandamanaji kuhudu uundwaji wa serikali ya mpito kuvunjika. Waandamanaji wamekuwa wakipiga kambi kwa karibu mwezi wa pili sasa, kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia, baada ya kuondolewa madarakani kwa[…]

13 wauawa katika shambulizi nchini Marekani.

Mtandao wa Marekani wa Gun Violence Archive umeonyesha kuwa shambulizi la kutumia silaha lililotokea katika fukwe za mapumziko mjini Virginia Marekani jana ni la 150 kufanyika kwa mwaka 2019 ambapo limesababisha vifo vya takriban watu kumi na watau tatu na wengine sita kujeruhiwa katika shambulizi la risasi lililotokea katika jengo la serikali. Mtandao huo umeripoti[…]