Serikali yasema hakuna njaa nchini Tathimini ya hali ya chakula katika Halmashauri 55 yaendelea

Serikali imesema hakuna njaa nchini, na kwa sasa hali ya chakula inaridhisha licha ya eneo kubwa la nchi kukosa mvua za msimu wa vuli ambazo zimesababisha ukame kwa baadhi ya maeneo. Kwa sasa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Shirika la Chakula Duniani, Taasisi ya Chakula na[…]

Rais Magufuli leo ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi

Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini. Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji Baridi mkoani Shinyanga. Rais Magufuli amesema Serikali haitayavumilia[…]

Marekani yathibitisha kufanya shambulizi la anga dhidi ya wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab nchini Somalia

Kituo cha jeshi la Marekani barani Afrika AFRICOM kimethibitisha kuwa kwa kushirikiana na majeshi ya Somalia na Umoja wa Afrika na washauri wa Marekani, jeshi hilo lilifanya shambulizi la anga dhidi ya kundi la Al-Shabaab ikiwa sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi. Jeshi hilo la AFRICOM limetoa taarifa ikisema, shambulizi hilo lilifanywa Januari 7 dhidi[…]

Mpango mkubwa wa Biashara barani Asia Tanzania yaingizwa kwenye mpango

Jitihada za Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan za kuiingiza Tanzania kwenye mpango mkubwa wa Biashara barani Asia, Mashariki ya kati, Ulaya na Afrika umefanikiwa baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi Saba kuingizwa katika mpango unaojulikana kama China One Belt, One Road Strategy. Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Makamu wa[…]