Waziri Mkuu awahimiza wakulima wasiogope kukopa kutoka mabenki

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wakubwa na wadogo wa miwa kwenye kiwanda cha sukari cha Manyara kuomba mikopo kutoka mabenki kama wanataka kuendeleza kilimo hicho lakini amewasisitiza kuwa ni muhimu kulipa. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani katika kijiji cha Matufa[…]

Bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 51 zimeteketezwa na TRA kushirikiana na TFDA Mbeya

BIDHAA zenye thamani ya shilingi milioni 51 Mkoani Mbeya, zikiwemo za chakula , vinywaji na sigara, ambazo hazifai kuingizwa nchini vimeteketezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA. Ernest Myenda ni Afisa Mfawidhi wa forodha Mbeya kitengo cha uzuiaji Magendo, anasema bidhaa zinazotekezwa ni pamoja na ambazo[…]

Serikali imeitaka menejimenti na wafanyakazi wa TTCL kubadilika katika utendaji wao wa kazi

Serikali imeitaka menejimenti na wafanyakazi wa shirika la umma la simu TTCL kubadilika katika utendaji wao wa kazi, kwa kuhakikisha huduma wanazotoa kwa wateja wao zinakuwa bora na zinakidhi mahitaji. Msisitizo huo umetolewa mjini Dodoma na Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akifungua duka la kisasa la kutolea huduma[…]