Mustakabali wa Kisiasa nchini Ethiopia.

Baada ya kuzindua mageuzi makubwa ya historia nchini Ethiopia, Waziri Mkuu Dkt. Abiy Ahmed, anakabiliwa na vitisho kufuatia mauaji ya mkuu wa jeshi na tuhuma kufuatia jaribio la mapinduzi katika Jimbo la Amhara, mambo ambayo yanaweza kupunguza kasi ya mchakato wake wa mageuzi. Waziri Mkuu Abiy amekuwa akipongezwa kuwa kiongozi mwenye maono, anayependa mageuzi ambaye[…]

Mwili wa Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi wazikwa.

Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani na waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo DRC Etienne Tshisekedi umezikwa leo nchini humo baada ya miaka miwili tangu afariki dunia Februari 2017 nchini Ubelgiji, mazishi ambayo yamehudhuriwa na viongozi sita kutoka mataifa ya Afrika. Maelfu ya waombolezaji walikusanyika katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa[…]

Sudan kushuhudia Maandamano makubwa.

Sudan inajiandaa kushuhudia Maandamano makubwa ya siku mbili ya Nchi nzima kuanzia leo,maandamano yenye lengo la kuongeza shinikizo zaidi kwa Utawala wa kijeshi kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. Viongozi walio chini ya mwamvuli wa waandamanaji, The Alliance for Freedom and Change na wanajeshi ambao walichukua madaraka mwezi mmoja uliopita baada ya kumuondoa Omar al-Bashir,[…]

Wakataa Wito wa kushiriki Maandamano.

Chama Kikuu cha Upinzani nchini Sudan pamoja na baadhi ya viongozi wa waandamanaji wamekataa wito wa kushiriki maandamano ya siku mbili yanayotarajiwa kufanyika Jumanne na Jumatano ya wiki hii kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa Utawala wa Kiraia,ambapo Msimamo huu wa upinzani ni ishara za kugawanyika ndani ya vuguvugu la mabadiliko linaloshiriki mazungumzo na baraza la[…]