BOMBADIER Q 400 imetua Iringa Kwa mara ya Kwanza.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ameongoza mamia ya wakazi wa Iringa wakiwemo wafanyabiashara wakubwa wa mazao ya Misitu na masuala ya utalii katika kuipokea ngege kubwa ya kwanza aina ya BOMBADIER Q 400 inayomilikiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutua katika uwanja wa ndege wa Nduli uliopo Manispaa ya Iringa kama ishara ya uzinduzi wa safari za ndege hizo mkoani humo.

Akiongea wakati wa zoezi hilo la uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa Nduli, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amesema ujio wa ndege hizo mkoani Iringa ni fursa kubwa kwa wananchi na hasa wafanyabiashara lakini pia amesema zitakuwa na tija katika kuikuza sekta ya utalii na hivyo kutimiza dhamira ya Rais Magufuli kuifanya Iringa kuwa kitovu cha utalii mikoa ya kusini.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa ndege wa Nduli Lydia Mwanisondol ameishukuru Serikali ya mkoa wa Iringa kwa juhudi zake za kufanya upanuzi wa uwanja huo huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Said Rubea akisema mambo yanayofanywa na viongozi wa serikali mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla ni historia kwa vizazi vijavyo.


Comments

comments