Wananchi wameshauriwa kutonunua maeneo ya Ardhi yasiyopimwa ili kuepuka Migogoro

Wananchi wameshauriwa kutonunua maeneo ya Ardhi yasiyopimwa ili kuepuka migogoro ya ardhi pamoja na kuvuruga mpango wa matumizi bora ya ardhi. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na mkurugenzi wa jiji hilo Godwin Kunambi wakati wa kikao kati ya madiwani, wakurugenzi wa makampuni ya upimaji wa ardhi pamoja na wenyeviti na watendaji wa serikali za mitaa[…]

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani achaguliwa kuwa Rais wa Halmashauri kuu Tume ya Ulaya .

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ,Ursula Von der Leyen, amechaguliwa Mkuu wa Tume ya Ulaya huku Bunge hilo likithibitisha uteuzi wake na hivo kuwa Mwanamke wa kwanza kuongoza taasisi Kuu ya Umoja wa Ulaya. Uthibitishwaji huo ulihitaji wingi wa kura 374 na Waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani anayendoka alipita kwa ziada ya kura tisa.[…]

Serikali imewataka wahandisi wa maji katika Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kutelekeza majukumu yao

Serikali imewataka wahandisi wa maji katika Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kutelekeza majukumu yao kwa weledi na maarifa, ili kuhakikisha miradi yote ya maji iliyoanzishwa nchini, inafanya kazi ya kuwahudumia wananchi. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji BW. JUMA AWESO, wakati alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha Mameneja wa RUWASA kwa[…]

Mtu mmoja amefariki Dunia na mamia ya Nyumba kuharibiwa baada ya tetemeko kubwa la Ardhi

Mtu mmoja amefariki dunia na mamia ya nyumba kuharibiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga Mashariki mwa Indonesia, kwa mujibu wa ripoti ya awali. Tetemeko hilo la ardhi lilitokea muda mfupi baada ya saa 12:00 jioni Kaskazini mwa Rasi ya Maluku, kwenye kina cha kilomita 10, na kusababisha hofu kwa wakazi na kulazimika kuyahama[…]

Ofisi ya Msitu wa Mbizi uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeanza mikakati ya kupambana na moto kichaa

Ofisi ya Msitu wa Mbizi uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeanza mikakati ya kupambana na moto kichaa unaotokea kila mwaka na kuharibu miti iliyopo katika shamba hilo licha ya kuwa msitu huo una vyanzo vya maji yanayotumika katika mji wa Sumbawanga kwa kuwakutanisha wakazi wa vijiji kumi na moja vinavyopakana na msitu wa[…]

Biashara katika Soko la Hisa la Dar es Salaam imeshuka kwa Asilimia 67 kwa thamani ya mauzo ya Hisa.

Biashara katika soko la Hisa la Dar es Salaam imeshuka kwa asilimia 67 kwa thamani ya mauzo ya hisa, baada ya kufanyika mauzo ya hisa milioni 2.9 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.4 kupitia mikupuo 156 wiki iliyopita. Meneja miradi wa soko hilo Emmanuel Nyalali akitoa ripoti ya mwenendo wa soko hilo kwa wiki iliyoishia[…]