Sumu Kuvu yasababisha Vifo Manyara.

Watoto watatu wamefariki dunia wilayani Kiteto na wengine watano wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Dodoma baada ya kula chakula ukiwemo ugali ambao inadaiwa unga wake umeathirika na sumu kuvu ambayo inapatikana kwenye mazao yasiyokaushwa au kukauka vizuri. Taarifa zinaleza kuwa watoto wawili wamepoteza maisha wakiwa katika hospitali ya wilaya ya Kiteto huku mmoja akipoteza[…]

Ziara iliyofanywa na Rais Dkt. Magufuli Namibia yaonesha mafanikio.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku mbili aliyofanya nchini Namibia kuanzia Mei 27 hadi 28 Mwaka 2019, kuanza kuonesha mafanikio baada ya kupokea ugeni kutoka Kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) Ltd inayomiliki kiwanda cha kuchakata[…]

TAKUKURU Yasisitiza Utaifishaji Mali Haramu.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Brigedia Jenerali JOHN MBUNGO, amesema serikali ya awamu ya tano itaendelea kutaifisha mali zinazopatikana kwa njia haramu ikiwemo ya RUSHWA kwa mujibu wa sheria ambapo hadi kufikia sasa zaidi ya shilingi Bilioni 14.7 zimerejeshwa serikalini pamoja na mali nyingine kwa kipindi cha[…]

Watanzania wamekumbushwa kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Taifa.

Wakati Tanzania ikiendelea kutekeleza sera ya viwanda inayolenga kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, watanzania wamekumbushwa kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Taifa, ili kuliwezesha Taifa kunufaika kiuchumi na rasilimali hizo. Ushauri huo umetolewa na jopo la wahariri wa vyombo mbalimbali habari nchini, baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha[…]

Treni ya Majaribio Mradi wa SGR yazinduliwa.

Serikali imeanza mchakato wa ununuzi wa vichwa 22 vya treni, mabehewa 1,430 ya mizigo na Mabehewa 60 ya Abiria vitakavyotumika kwenye uendeshaji wa Reli ya kisasa ya SGR ambayo ujenzi wake unaendelea. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amefahamisha mpango huo wakati akizindua Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi[…]

Wananchi watakiwa kulinda Maliasili.

Katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira unayoyakabili baadhi ya maeneo ya hifadhi za Taifa, Wizara ya maliasili na utalii imewataka wananchi kulinda maliasili na hifadhi zinazowazunguka, ili kuviwezesha vizazi vya sasa na vijavyo kunufaika na rasilimali hiyo. Wizara hiyo imetoa agizo hilo leo Jijini Mwanza, kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya wizara Dkt. Hamis Kigwangala.[…]